STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 17 Aprili 2015

Etoile Du Sahel Yatua Dar Kwa ‘Mkwara’ Mzito Wa Kuimaliza Yanga

Wachezaji wa Etoile du Sahel wakitoka nje ya uwanja wa ndege muda mfupi baada ya kuwasili leo alfajiri
Wachezaji wa Etoile du Sahel wakitoka nje ya uwanja wa ndege muda mfupi baada ya kuwasili leo alfajiri
Timu ya Etoile du Sahel tayari imeshawasili jijini Dar es Salaam ikitokea Tunisia kwa ajili ya mechi ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao Yanga SC mchezo utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa.
Mchezaji wa Etoile du Sahel ikionesha vidole vitatu kuashiria wataichakaza Yanga kwa goli taru
Mchezaji wa Etoile du Sahel ikionesha vidole vitatu kuashiria wataichakaza Yanga kwa goli tatu
Etoile imewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alfajiri ya leo wakiwa na msafara wenye jumla ya watu 56 kati yao wachezaji ni 19, benchi la ufundi likiwa na watu 13, waandishi wa habari 12 na wengine 10.
Wachezaji wa Etoile du Sahel wakiingia kwenye basi tayari kuelekea kwenye hoteli waliyofikia
Wachezaji wa Etoile du Sahel wakiingia kwenye basi tayari kuelekea kwenye hoteli waliyofikia
Msafara huo umepokelewa na afisa ahabari wa Yanga SC Jerry Muro ambaye aliwasindikiza moja kwa moja mpaka kwenye hoteli waliyofikia ambayo ni Ledger Plaza na baadae watafanya mazoezi yao kwenye uwanja wa Taifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox