STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 17 Aprili 2015

KUELEKEA KUIVAA CHELSEA....VAN GAAL KICHWA CHAMUUMA

Chelsea na Manchester United zitakutana kesho Stamford Bridge kuchuana katika mechi ya ligi kuu England inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi duniani.
Man United wataingia katika mechi hiyo wakiwa na rekodi nzuri ya kushinda mechi sita, lakini wachezaji muhimu watakosekana katika kikosi cha kocha Mholanzi, Louis van Gaal.
Wayne Rooney atalazimika kurudi zaidi katika majukumu ya kiungo baada ya Michael Carrick na Daley Blind kuondolewa katika kikosi kitakachovaana na vinara wa ligi guu, Chelsea.
Pia mlinzi wa kati Phil Jones na Marcos Rojo wataikosa mechi hiyo ,  Jonny Evans anamalizia adhabu yake ya kufungiwa mechi sita na tayari Van Gaal ameshaanza kuonesha wasiwasi baada ya kueleza kuwa yupo katika mazingira magumu kwa kuwakosa wachezaji hao muhimu.

Jones na Blind walijeruhiwa na Vicent Kompany kwenye mechi ya mahasimu wawili wa jiji la Manchester, Manchester United na Manchester City.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox