STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 3 Septemba 2015

CHUNG AITUHUMU AFC KUMFANYIA NDIVYO SIVYO.......


MGOMBEA urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutoka Korea Kusini, Chung Mong-Joon amelituhumu Shirikisho la Soka la Asia-AFC kwa kile alichokiita udanganyifu wa uchaguzi kwa kumuunga mkono mgombea mwenzake Michel Platini.

 Chung amesema AFC ambayo rais wake Sheikh Salman bin Ibrahim Al Khalifa ameshajitokeza hadharani kumuunga mkono Platini, amesambaza barua kwa kila mjumbe wa AFC kasoro Korea Kusini na Jordan ili kuwashawishi wamuunge mkono Platini. 

Prince Ali bin Hussein wa Jordan pia yuko katika kinyang’anyiro hicho cha kuchukua nafasi ya Sepp Blatter kama rais wa FIFA.

 Chung amesema kitendo kinachofanywa na rais wa AFC ni ukiukwaji wa sheria za uchaguzi kwani kinakandamiza wagombea wengine. Uchaguzi wa FIFA unatarajiwa kufanyika Februari 26 mwakani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox