STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 3 Septemba 2015

MKWASA AMPA TABU OLISEH............




KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles, Sunday Oliseh amedai kuvutiwa na kiwango cha timu ya taifa ya Tanzania-Taifa Stars pamoja na nafasi waliyopo katika kundi lao.

 Oliseh amekuwa akitizama mikanda ya mechi mbalimbali za Stars zilizopita ili kung’amua hilo na lile kabla ya kukutana na kikosi hicho kilicho chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa Jumamosi hii. 

Hata hivyo, Oliseh amekiri kuwa mechi nyingi zilizopita za Stars alizotizama zilikuwa sio zinazosimamiwa na kocha wa sasa Mkwasa hivyo bado yuko gizani kwakuwa hazifahamu mbinu za kocha huyo.

 Oliseh amesema Stars ni timu inayocheza kwa nguvu na kuna baadhi baadhi ya mambo mengine wanaweza kuyaona kwa mara ya kwanza kwani hajui mbinu mpya alizonazo Mkwasa. 

Super Eagles wamewasili jijini Dar es Salaam leo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox