MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc
leo asubuhi wamecheza mechi ya kujipima
uwezo dhidi ya Ruvu Shooting katika dimba la Azam Complex, Mbande, nje kidogo
ya jiji la Dar es salaam.
Hadi dakika 90 zinamalizika, Azam fc walikuwa
mbele kwa bao moja lililofungwa kipindi cha pili na kinda wake, Bryson Raphael.
Mechi hiyo ilitumika na makocha wa timu zote, Joseph Marius Omog wa Azam na Tom Alex Olaba Ruvu Shooting ili kuangalia kama wachezaji wao wanashika mafundisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni