Yaya Toure akitumbukiza penati yake wavuni kuibeba Manchester City dhidi ya Everton |
Toure alifunga bao hilo katika dakika ya 24 baada ya Phil Jagielka kumchezea rafu James Milner na yeye kutofanya ajizi kuukwamisha mpira kimiani na kuifanya City ambao ni mabingwa watetezi kufikisha pointi 33 na kung'ang'ania nafasi ya pili nyuma ya Chelsea ambayo mapema leo mchana ilikubali kipigio cha mabao 2-1 toka kwa wenyeji wao Newcastle United na kusitishiwa mfululizo wake wa ushindi katika msimu huu.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea siku ya Jumatatu kwa pambano moja tu litakaloikutanisha Southmapton dhidi ya Mashetani Wekundu, Manchester United.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni