MENEJA wa klabu ya
Chelsea, Jose Mourinho amesema mshambuliaji wake Didier Drogba bado
atakuwa na kazi Stamford Bridge wakati akiamua kustaafu rasmi kucheza
soka. Drogba mwenye umri wa miaka 36 kwasasa anaichezea kwa mara ya pili
klabu hiyo huku akifunga bao katika mchezo wa jana ambao Chelsea
waliibugiza Tottenham Hotspurs kwa mabao 3-0. Akihojiwa Mourinho amesema
jambo ni kwamba nyota huyo atamalizia soka lake akiwa na Chelsea na
inavyoonekana anaweza kubakia akifanya mambo mengine pindi
atakapostaafu. Drogba amefanikiwa kushinda mataji 10 akiwa na Chelsea
mara ya kwanza kati ya mwaka 2004 mpaka 2012 huku akifunga mabao 157
katika mechi 341 alizocheza. Nyota huyo alijiunga tena na Chelsea katika
kipindi cha majira ya kiangazi mwaka huu baada ya kuondoka klabu ya
Galatasaray ya Uturuki.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Alhamisi, 4 Desemba 2014
MOURINHO KUMPA KIBARUA DROGBA AKISTAAFU SOKA.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni