KLABU ya Chelsea imepata
pigo baada ya golikipa wake Thibaut Courtois kupata majeruhi ya msuli
kuelekea katika mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Hul City. Golikipa
huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anaungana na Cesc Fabregas anayetumikia
adhabu kuwa wachezaji ambao wataukosa mchezo huo wakati Chelsea
wakijaribu kurejesha makali yao baada ya kipigo kutoka kwa Newcastle
United mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza
na wanahabari meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema Courtois alikuwa
na matatizo madogo wakati wa mazoezi hivyo hatakuwepo katika mchezo wa
kesho. Mourinho
aliendelea kudai kuwa Fabregas amekuwa na msaada mkubwa katika kikosi
chake lakini hawatakuwa naye katika mchezo wa kesho akitumikia adhabu
yake ila wana wachezaji wengine anaowaamini. Mourinho
sasa atalazimika kuendelea kumtumia Petr Cech ambaye alimtumia pia
katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon
Jumatano iliyopita.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 12 Desemba 2014
PIGO: CHELSEA KUMKOSA COURTOIS KESHO.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni