KLABU ya Arsenal
itajitupa tena uwanjani kesho kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya
Stoke City bila ya winga wake Theo Walcott ambaye bado anauguza majeraha
ya msuli. Walcott ambaye alirejea tena uwanjani na kucheza mechi mbili
akitokea benchi Novemba mwaka huu naada ya kujiuguza kwa karibu mwaka
mzima majeraha ya goti, aliumia msuli wakati akiwa katika majukumu ya
kimataifa. Akizungumza na wana habari Wenger amesema Walcott alichomwa
sindano leo hivyo hatakuwepo katika mchezo kesho na kuendelea kudai kuwa
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray nao unaweza kuwa
mapema sana kwake. Beki wa kushoto Nacho Monreal
pia
atakosa mchezo huo baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Southampton
katikati ya wiki lakini golikipa Wojciech Szczesny yeye atakuwepo baada
ya kuanza mazoezi. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa Arsenal kwani
toka Stoke wamepanda daraja mwaka 2008, washika bunduki hao wamefanikiwa
kuwafunga mara moja pekee nyumbani kwao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni