MANCHESTER
CITY ikiwa uwanja wa nyumbani wa Etihad imechapwa mabao 2-1 na wakali
wa Catalunya, FC Barcelona katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 ya ligi
ya mabingwa Ulaya.
Luis
Suarez amepiga magoli mawili katika dakika ya 16' na 30', akipewa pasi
za mwisho na Jord Alba wakati Sergio Aguero ameifunga City bao la
kufutia machozi katika dakika ya 69' akimalizia pasi ya David Silva.
Dakika tano baada ya bao hilo, Gael Clichy alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonesha njano ya kwanza.
Lionel Messi amekosa penalti dakika ya 90'.
Takwimu za mchezo zinaonesha kuwa Barcelona wameongoza umiliki wa mpira kwa asilimia 61 kwa 39 za Man City.
Barcelona wamepiga mashuti 5 yaliyolenga lango dhidi ya 4 ya Man City.
Mashuti yasiyolenga lango kwa Barca ni 6 wakati Man City wamepiga 5.
Man City wamefanikiwa kupiga kona 9, Barcelona 4. Wenyeji hawajaotea, Barca wameotea mara 12.
Kikosi cha Man City kimefanya madhambi mara 13 wakati Barcelona wamefanya mara 12.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni