Kikosi
cha Yanga kinatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Botswana kwa ajili
ya kuwavaa BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
Yanga itaondoka nchini ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na memba wa benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.
Katika mechi ya kwanza, Yanga ikiwa nyumbani ilishinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe.
Safari hiyo ya Yanga kwenda Botswana ni kumalizia mechi hiyo ya pili.
Kabla
ya safari hiyo, Yanga ikiongozwa na Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der
Pluijm ilishinda mechi tatu ikianza kwa kuitwanga BDF XI kabla ya
kuhamia kwenye ligi.
Katika mechi za Ligi Kuu Bara, Yanga ilianza kwa kuitungua Prisons kwa mabao 2-0, halafu ikageuka na kuichapa Mbeya City kwa mabao 3-1 kuthibitisha kuwa haikubahatisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni