KIJANA
Nasry Daudi Aziz aliyezaliwa Agosti 21, 2001 amechaguliwa kujiunga na
kituo cha kukuza vipaji cha Aspire Football Dream kilichopo katika mji
wa Dakar nchini Senegal.
Mradi
wa Aspire nchini ulianza mchakato wa kusaka vijana mwezi Machi - Mei,
2014 ambapo vijana wengi walijitokeza na kuchaguliwa vijana 14 ambao
walikwenda katika mchujo mwingine uliofanyika nchini Uganda
uliowashirikisha vijana zaidi ya 50.
Kijana
huyo ni miongoni mwa wachezaji 17 waliochaguliwa kati ya vijana 34
walikuwepo nchini Senegal kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo kulikuwa na
vijana wengi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Amerika ya Kusini.
Kituo
cha Aspire kilichopo Dakar nchini Senegal ni miongoni mwa vituo viwili
vinavyoongozwa na mtoto wa mfalme wa Qatar na timu ya Barcelona, kituo
kingine kipo mjini Doha.
Nasry
Daud Aziz anatarajiwa kuondoka nchini Februari 28 mwaka huu kuelekea
Dakar ambapo atakua kwenye kituo hicho kwa mkataba wa miaka miatano.
Kutoka
nchini Tanzania Nasry anakua ni kijana wa tatu kujiunga na kituo hicho,
wengine ni Matine Taganzi na Orgenes Morrel ambaye aliitwa kwenye timu
ya Taifa Stars maboresho na kocha Mart Nooj.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni