Kocha
Mkuu wa Tanzania Prisons, David Mwamaja amesema wamelazimishwa na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kucheza mechi Alhamisi dhidi ya Yanga
SC mjini Mbeya.
Mwamaja amesema kikosi chake kilichokuwa kimeweka kambi jijini hapa
kujiandaa kwa mechi ya mwishoni mwa wiki hii dhidi ya mabingwa watetezi
Azam FC, kimelazimika kurejea jijini Mbeya baada ya kutakiwa kufanya
hivyo na TFF.
Amesema kikosi chake kimetua nyumbani, Mbeya leo jioni, tayari kuwavaa Yanga SC ambao wametamba moto wao hauzimiki kwa sasa,
“Timu ilikuwa Dar es salaam tukijiandaa kwa mechi dhidi ya Azam, lakini
tumelazimishwa kurejea Dar es Salaam kucheza dhidi ya Yanga," amesema
kocha huyo aliyewahi kuinoa Simba SC mwaka 1999 wakati Mtibwa Sugar FC
wakitwaa taji la kwanza la Tanzania Bara.
Mwamaja ambaye kikosi chake kiko mkiani mwa msimamo, amesema hana hofu dhidi ya kikosi cha Yanga SC kwa kuwa anakifahamu vyema.
"Yanga tunawajua na wao pia wanajua moto wetu. Tumekuwa na matokeo ya
sare nyingi, lakini sare si mbaya, bunduki zetu ziko sawa kwa ajili ya
mechi hiyo," amesema zaidi Mwamaja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni