STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 17 Mei 2015

Familia kuamua hatma ya De Gea kubaki au kung’oka Man U

Gazeti lililoripoti habari ya De Gea kuamulia na familia pamoja na mke wake

Gazeti lililoripoti habari ya De Gea kuamulia na familia pamoja na mke wake


Golikipa wa Manchester United David De Gea akia pamoja na mkewake Edurne Garcia
Golikipa wa Manchester United David De Gea akiwa pamoja na mkewake Edurne Garcia

Gazeti la leo Jumapili la The Star limekuja na stori kwamba hatma ya golikipa David De Gea kubaki Manchester United au kuelekea Real Madrid itaamuliwa na familia yake.

Kwa mujibu wa gazeti hilo la udaku, De Gea atafanya maamuzi yake wakati wa likizo baada ya kuitisha kikao cha familia yake mjini Madrid na inaelezwa kuwa kipa huyo anaheshimu mno mawazo ya familia katika maamuzi yake.

The Star limeripoti; “Golikipa wa Manchester United bado hajafikia maamuzi ya kusaini mkataba wa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki akiwa Old Trafford au kujiunga na Real Madrid”.

De Gea mwenye umri wa miaka 24, ana familia yake Hispania ambayo anaheshimu sana mawazo yake na ataomba maoni yao kabla ya kufikia maamuzi.

Mkutano huo unatarajia kufanyika baada ya ligi kuu England kumalizika na utamuhusisha mpenzi wake anayeishi Madrid, Edurne Garcia.

Hata hivyo, gazeti la Marca lilichapisha stori mwishoni mwa wiki iliyopita likidai De Gea tayari ameshamalizana na Real Madrid.

Kichwa kikubwa kiliandikwa ‘Trato Hecho’ katika ukurasa wa mbele pamoja na picha ya kipa wa Manchester United, David De Gea  kikimaanisha ‘Done Deal’, yaani dili likemakilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox