Paris St-Germain wamefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu Ufaransa kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya kupata ushindi dhidi ya Montpellier.
PSG walikuwa wakihitaji pointi moja tu ili kuweza kufanikiwa kunyakua taji ilo na kuwa klabu ya nne nchini Ufaransa kuweza kunyakua taji hili mara tatu mfululizo.
Kiungo wa Ufaransa Blaise Matuidi aliweza kufunga goli moja pamoja na mshambuliaji raia wa Argentina Ezequiel Lavezzi.
Montpeller walijibu mashambulizi kwa kufanikiwa kupata bao moja lililofungwa na mshambuliaji wao Anthony Mounier, ila vijana wa Laurent Blanc waliweza kulinda ushindi wao mpaka mwisho.
Baada ya ushindi huo PSG sasa wanaweza kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja ikiwa watafanikiwa kuchukua taji la French Cup na French League Cup.
PSG walikuwa bila ya mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic ambaye alikua akisumbliwa na maumivu ya paja, kukosekana kwake kulibadili kidogo uchezaji na makali ya PSG kwa ujumla.
PSG katika mechi zao nne zilizopita wamekua na rekodi nzuri ya ufungaji wakifanikiwa kufunga magoli 17, huku wakipata ushindi mnono dhidi ya Lille na Guingamp kwa kuweza kuwafunga magoli sita kwa kila timu.
ORODHA YA TIMU ZILIZO CHUKUA UBINGWA WA LIGUE 1 MARA NYINGI::
1.Marseille (10)
1929, 1937, 1948, 1971, 1972, 1989, 1990, 1991, 1992, 2010
2.Saint-Étienne (10)
1957, 1964, 1967, 1968, 1969, 1970, 1974, 1975, 1976, 1981
3.Nantes (8)
1965, 1966, 1973, 1977, 1980, 1983, 1995, 2001
4.AS Monaco (7)
1961, 1963, 1978, 1982, 1988, 1997, 2000
5.Lyon (7)
2002, 2003, 2004, 2005, 2006, 2007, 2008
6.Stade de Reims (6)
1949, 1953, 1955, 1958, 1960, 1962
7.Bordeaux (6)
1950, 1984, 1985, 1987, 1999, 2009
8.Standard Athletic Club (5)
1894, 1895, 1897, 1898, 1901
9.Roubaix (5)
1902, 1903, 1904, 1906, 1908
10.Paris Saint-Germain (5)
1986, 1994, 2013, 2014, 2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni