Paris
St-Germain wamefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu Ufaransa kwa msimu wa
tatu mfululizo baada ya kupata ushindi dhidi ya Montpellier.
PSG
walikuwa wakihitaji pointi moja tu ili kuweza kufanikiwa kunyakua taji
ilo na kuwa klabu ya nne nchini Ufaransa kuweza kunyakua taji hili mara
tatu mfululizo.
Kiungo wa Ufaransa Blaise Matuidi aliweza kufunga goli moja pamoja na mshambuliaji raia wa Argentina Ezequiel Lavezzi.
Montpeller
walijibu mashambulizi kwa kufanikiwa kupata bao moja lililofungwa na
mshambuliaji wao Anthony Mounier, ila vijana wa Laurent Blanc waliweza
kulinda ushindi wao mpaka mwisho.
Baada
ya ushindi huo PSG sasa wanaweza kubeba mataji matatu ndani ya msimu
mmoja ikiwa watafanikiwa kuchukua taji la French Cup na French League
Cup.
PSG
walikuwa bila ya mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic ambaye alikua
akisumbliwa na maumivu ya paja, kukosekana kwake kulibadili kidogo
uchezaji na makali ya PSG kwa ujumla.
PSG
katika mechi zao nne zilizopita wamekua na rekodi nzuri ya ufungaji
wakifanikiwa kufunga magoli 17, huku wakipata ushindi mnono dhidi ya
Lille na Guingamp kwa kuweza kuwafunga magoli sita kwa kila timu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni