WACHEZAJI wa Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho na Mliberia, Kpah Sherman, wamewekwa sokoni ili kuwapisha wachezaji wengine wa kigeni katika kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga
ipo katika mikakati ya kusajili wachezaji wa kiwango cha kimataifa ili
waweze kufanya kweli kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Akifanya
mahojiano na gazeti la BINGWA jana, Katibu Mkuu Yanga, Jonas Tiboroha
amesema kuwa wamedhamiria kufanya kweli kwenye usajili wao kuelekea
msimu ujao, hivyo moja ya vigezo ambavyo uongozi wa timu hiyo
unavizingatia ni pamoja na kusajili wachezaji watakaoendana na hadhi ya
klabu hiyo.
“Tumedhamiria
kufanya usajili wa nguvu msimu ujao, moja ya mikakati yetu ni
kuhakikisha tunapata wachezaji wapya wa kigeni ambao watakuwa na uwezo
mkubwa wa kuipa heshima Yanga na sio kusajili ovyo tena,” alisema
Tiboroha.
Alisema
kutokana na hilo, wameamua kuwaweka sokoni kiungo mshambuliaji,
Coutinho na mshambuliaji, Sherman tayari kuwapisha wengine kuziba nafasi
zao baada ya klabu yao kutoridhishwa na uwezo wa wawili hao.
Chanzo:Bingwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni