RASMI!
kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF
inatarajiwa kukutana jumapili mei 24 mwaka huu ikiwa ni kikao cha
kawaida cha kamati hiyo.
Moja
ya ajenda katika kikao hicho itakua ni kupokea na kujadili mienendo,
maandalizi na maendeleo ya timu zetu za Taifa za mpira wa miguu nchini
hususani Taifa Stars.
Stars
imelitia aibu soka la Tanzania baada ya kufungwa na nchi vibonde za
Swaziland na Madagascar na kutupwa nje ya michuano ya Cosafa.
Kupitia
akaunti yake ya Twitter (Rejea habari za mwanzo za mtandao huu), Rais
wa TFF amesikitishwa na matokeo ya Stars akidai kuwa wamewekeza fedha
nyingi lakini matokeo si mazuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni