CARLO ANCELOTTI KUBWAGA MANYANGA REAL MADRID JUMAPILI, MRITHI WAKE HUYU HAPA.....
GAZETI
la kila siku la Hispania, AS, limeikariri Sky Sport Italia wakiripoti
kuwa Carlo Ancelotti anaondoka Real Madrid jumapili ya juma hili.
Real Madrid watahitimisha msimu wa 2014-15 bila kombe lolote na hali hiyo ya ukame imetia mchanga kibarua cha Ancelotti.
AS
wanaripoti kwamba baada ya msimu kuisha, Ancelotti atakutana na rais wa
klabu, Florentino Perez na wawili hao kwa pamoja wataafikiana kuvubja
mkataba unaotakiwa kumalizika juni 30 mwaka 2016.
Wakati
Ancelotti akiondoka Bernabeu, tetesi zinasema Real inamfukuzia Benitez
au kocha wa sasa anayeondoka Borussia Dortmund, Jurgen Klopp.
Benitez,
kocha wa zamani wa timu ya vijana ya Real Madrid ambaye pia aliwapa
makombe mawili ya La Liga, Valencia anapewa nafasi kubwa zaidi ya
kumrithi Ancelotti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni