STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 21 Oktoba 2015

YANGA WAICHAPA TOTO, MNYAMA AFIA SOKOINE KULE MBEYA, MAGURI APIGA 2 STAND IKISHINDA 3, MATOKEO YOTE YAKO HAPA

Simba imepoteza mechi yake ya pili ya Ligi Kuu Bara ndani ya mechi saba tu.

Simba ilipoteza mechi yake ya kwanza ikicheza mechi yake ya nne ya ligi ilipokutana na mabingwa watetezi Yanga iliyowachapa bao 2-0.

Ikiwa ugenini, Simba imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wake Prisons ya Mbeya ambayo imetoka kupoteza me
chi yake kwa kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Stand Unitd.

Timu hizo zilimaliza kipindi cha kwanza kwa sare ya bila bao kwenye Uwanja wa Sokoine, lakini Prisons wakafanikiwa kupata bao katika kipindi cha pili kilichotawaliwa na ubabe na tafrani.


 
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justice Majabvi,  Simon Sserunkuma/Mwinyi Kazimoto, Awadh Juma/Said Ndemla, Pape Ndaw, Joseph Kimwaga na Peter Mwalyazi/Ibrahim Hajib.

 
Prisons; Aron Kalambo, Laurian Mpalile/Beno Kakolanya, Salum Kimenya, Nurdin Chona, James Mwasote, Jumanne Elfadhili, Lambart Sabiyanka, Juma Seif ‘Kijiko’/Ally Milanzi, Mohammed Mkopi, Jeremiah Juma na Benjamin Asukile.


Na kule Dar es salaam
YANGA SC imejiweka vizuri katika kiti cha usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 4-1 Toto Africans ya Mwanza jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
 
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 19 baada ya mechi saba, ikiwazidi kwa pointi tatu Azam FC ambao kesho wanacheza mechi ya saba dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara. 

 
Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na beki wa kulia, Juma Abdul dakika ya tisa kwa shuti kali umbali wa zaidi ya mita 20 akimaizia kona ya Haruna Niyonzima.


Hata hivyo, Yanga SC wangeweza kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa wanaongoza kwa mabao zaidi kama wangetumia vizuri nafasi zote walizotengeneza, ikiwemo penalti ambayo alikosa Mzimbabwe Donald Ngoma.
 
Ngoma alikosa penalti hiyo dakika ya 45 ikipanguliwa na kipa wa Toto, Mussa Mohammed baada ya yeye mwenyewe kumnawisha mpira beki Carlos Protas na refa Ahmada Simba wa Kagera akaamuru pigo hilo.

 
Katika kipindi cha kwanza, Toto walifanya shambulizi moja tu la maana, Miraji Athumani ‘Madenge’ akishindwa kumalizia vizuri pasi ya Edward Christopher dakika ya 42 kwa kumpa nafasi kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ kupangua.

 
Kipindi cha pili, Yanga SC walianza na mabadiliko Juma Abdul akimpisha Simon Msuva ambaye alikwenda kufunga bao la pili dakika ya 49.


Toto Africans ilipata bao lake dakika ya 62 kupitia kwa Miraj Athumani ‘Madenge’ kwa kichwa akimalizia mpira ulioparazwa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Bernad Evarigetus.
 
Mrundi Amissi Tambwe aliipatia Yanga SC bao la tatu dakika ya 81 akimalizia krosi ya Simon Msuva ambaye alifunga bao la nne dakika ya 90 akimalizia pasi ya Mbrazil Andrey Coutinho.

 
Beki wa Toto, Hassan Khatib alionyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 90 na ushei kwa utovu wa nidhamu na kutolewa kwa kadi nyekundu.

 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Simon Msuva dk46, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan/Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Godfrey Mwashiuya/Andrey Coutinho.  

 
Toto Africans; Mussa Mohammed, Hassan Khatib, Robert Magadula/Miraj Makka, Hamisi Kasanga, Carlos Protas, Salimn Hoza/William Kimanzi, Japhet Vedastus/Jaffar Mohammed, Abdallah Seseme, Evarigetus Bernad, Edward Christopher na Miraji Athumani.


Kutoka Tanga
Mabingwa wazamani wa ligi kuu ya vodacom Coastal union imefanikiwa kufunga goli lao la kwanza katika msimu huu wa ligi kuu ya vodacom baada ya kucheza michezo 7 ya ligi hiyo.

Coastal union leo walikuwa katika uwanja wa Mkwakwani kuwakabili Kagera sugar ya mkoani Kagera ikiwa chini ya kocha wa muda baada ya kocha wao mkuu Salum Mayanja kumtimua.

Goli hilo la kwanza kwa Coastal union lilifungwa katika dakika ya 13 kupitia kwa Yusuf Chuma na kuipa pointi tatu muhimu Coastal union mbele ya Kagera Sugar.

Katika mchezo huo Coastal union waliibuka na ushindi wa goli hilo 1 na kuvuna pointi zote tatu. 
 
 
 


Shinyanga 
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Elias Maguri amefunga mabao mawili dakika za 47 na 60 timu yake, Stand United ikishinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Kambarage Shinyanga, bao lingine likifungwa na Pastory Athanas dakika ya 66.
FTSTAND UNITED 3 : 0MAJIMAJI
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox