STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 20 Oktoba 2015

LIGI KUU TANZANIA: BAADA YA MICHEZO YA MWISHO WA WIKI, HIKI NDIO KIKOSI BORA CHA VPL



1.Aishi Manula (Golikipa)
Kipa namba moja wa klabu ya Azam FC, ametoa mchango mkubwa kwa timu yake Jumamosi ilipokuwa ikipambana na Yanga Jumamosi iliyopita ambapo aliweza kupangua penalti ya Thabani Kamusoko, na kuiwezesha timu yake kupata sare ya 1-1. Anastahili kuwa kipa wa wiki katika Ligi Kuu ya Vodacom

2.Juma Abduli
Mlinzi huyu wa kulia wa Yanga amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake, naye ndiye aliyepiga krosi ya bao la Yanga lililofungwa na Donald Ngoma. Beki namba mbili!

3.Mohamed Hussein ‘Tshabalala’
Beki mwenye uwezo mkubwa kutoka klabu ya Simba amekuwa na mchango mkubwa kwa timu hiyo na kuchangia kwa asilimia kubwa ushindi wa bao 1-0 walioupata Jumamosi dhidi ya Mbeya City, ana haki ya kuzawadiwa namba 3 kikosi cha wiki.

4.Kelvin Yondan
Beki wa kati wa Yanga ambaye kwa sasa amekuwa kwenye kiwango bora akitoa mchango mkubwa kwa klabu hiyo aliyojiunga nayo akitokea Simba Jumamosi, alicheza vizuri japo waliambulia sare ya 1-1 na Azam FC. Hakuna ubishi nambari nne hana mpinzani katika kikosi hiki.

5.Rajabu Zahir
Beki kitasa wa Stand United ya Shinyanga ameweza kutoa mchango mkubwa kwa timu yake na kuwezesha kumaliza dakika 90 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons Jumamosi, anapata tano

6.Himid Mao
Kiungo mkabaji wa Azam FC, ametoa mchango mkubwa kwa timu yake dhidi ya Yanga Jumamosi na uwezo wake wa kukaba ulisaidia kupunguza kasi ya washambuliaji wa Yanga kuliandama lango lao. Namba sita.

7.Twaha Shekuhe
Winga wa Coastal Union ya Tanga ambaye pamoja na timu yake kuwa na mwenendo mbaya tangu kuanza kwa msimu huu lakini amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuipigania timu yake ikiwepo kwenye mchezo wao Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar….namba saba mahali pake.

8.Salum Abubakar ‘Sure Boy’
Kiungo wa Azam FC ambaye alicheza vizuri kwenye eneo la kiungo na kuwavuruga vioungo wa Yanga japo mipango yake ilikuwa ikikwamishwa na mabeki wa Yanga. Nane!

9.Elias Maguri
Straika wa Stand United aliyeanza kwa kasi msimu huu na sasa anaongoza kwenye orodha ya ufungaji akiwa na mabao sita yakiwemo mabao mawili aliyoyafunga Jumamosi wakati timu yake ilipoifunga Prisons mabao 3-0. Anapata 9.

10.Donald Ngoma
Mshambuliaji mrefu wa Yanga ambaye katika mechi sita za awali ameonyesha kama kweli yeye ni mkali baada ya kuonyesha uwezo mkubwa Ligi Kuu ya Vodacom na kufunga mabao matano kwenye mechi ngumu ikiwemo ile ya Jumamosi dhidi ya Azam FC. Kumi!

11.Julias Mrope
Winga wa kushoto wa Mwadui FC, ambaye ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu, wikiendi hii mchezaji huyo wa zamani wa klabu za Simba na Yanga amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha Jamhuri Khwelo ‘Julio’ anapata 11.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox