MARA
tu baada ya sare ya 2-2 na wenyeji Tanzania, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, wachezaji wa Algeria walielekea kwenye hoteli ya Hyatt Regency
(Kilimanjaro Kempinsky) kwa ajili ya mapumziko mafupi.
Baada
ya mapumziko yao ya takriban saa mbili, walioga na kuelekea Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam ambako ndege
yao waliyokuja nayo ilikuwa inawasubiri wao tu.
Wakapanda ndege hiyo na kwenda moja kwa moja nyumbani, Algiers ambako walifika siku hiyo baada ya saa sita za angani.
Na
baada ya kufika Algiers, siku ilifyofuata wakaanza mazoezi kwa ajili ya
mchezo ujao wakati huo huo, wachezaji watatu ambao hawakuwepo katika
mchezo wa kwanza wakaitwa kutoka Ulaya kuja kuongeza nguvu.
Hao
ni Mwanasoka Bora Afrika wa BBC mwaka jana, Yacine Brahimi, Belkaroui
Hichem na Boudebouz Ryad, ambao wote walifika Jumapili jioni na Jumatatu
walifanya mazoezi na wenzao.
VIPI TAIFA STARS?
Kwa
upande wa Taifa Stars, mara tu baada ya mchezo wa kwanza walikuwa wana
kikao kifupi na Makamu wa Rais Dk. Samia Hassan Suluhu pale Uwanja wa
Taifa.
Baada
ya hapo, wakarejea kambini kwao, hoteli ya Serena ambako baadaye tena
wakawa na kikao na Kamati ya Taifa Stars, iliyowaahidi Sh. Milioni 500
iwapo wangeitoa Algeria.
Kamati
ya Taifa Stars iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy
Mecky Sadick waliwaweka mezani wachezaji kwa zaidi ya lisaa limoja na
nusu wakifanya nao mazungumzo baada ya chakula cha usiku.
Kutoka
hapo, wachezaji wakaenda kulala saa mbili tu kabla ya kuamshwa kwa
safari ya JNIA kusubiri ndege ya shirika la Uturuki, waende Algiers
kupitia Istanbul.
Wachezaji
walikaa JNIA kwa saa mbili wakisubiri kuingia kwenye ndege ya Uturuki
na kusafiri kwa saa nane kasoro kidogo hadi Istanbul, ambako walikaa kwa
saa mbili kabla ya kuunganisha ndege kwenda Algiers ambako walitumia
saa tatu.
Msafara
wa Taifa Stars ulifika Algiers saa 12 jioni za huko sawa na saa mbili
usiku kwa saa za nyumbani- yaani baada ya kucha na kutwa za safari.
Kutoka
hapo, wakasafiri kwa basi kwa zaidi ya saa moja kwenda mjini Blida
ambako baada ya kufika hawakupata muda wa mazoezi siku hiyo yote ya
Jumapili.
Siku
iliyofuata ya Jumatatu, kutokana na uchovu wa safari, wachezaji
walishinda hotelini tu kabla ya kwenda kufanya mazoezi kidogo tu kwa saa
moja usiku wake Uwanja wa Mustapha Tchaker.
Jumanne
asubuhi makocha Charles Boniface Mkwasa na Msaidizi wake, Hemed Morocco
waliongozana na wachezaji wao kufanya matembezi ya nusu saa kwenye
mitaa ya jirani na hoteli yao mjini Blida.
Baada
ya hapo, wakarudi kupata kifungua kinywa, baadaye chakula cha mchana na
cha jioni pamoja na kupumzika kabla ya kwenda uwanjani kwa ajili ya
mchezo wa marudiano.
Ni
mchezo wa ugenini ambao Taifa Stars ilihitaji ushindi ili kuingia hatua
ya mwisho ya mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Algeria ambayo inatuacha
mbali kwa kila kitu kiuwezo na uwekezaji kwenye soka.
Baada
ya dakika 45 tu, tayari Stars ilikuwa imekwishapigwa mabao matatu na
kipindi cha pili wakaongezwa manne na kulala kwa 7-0, hivyo kutolewa kwa
jumla ya mabao 9-2.
TUMEKOSEA WAPI?
Ni
kweli Algeria wanatuzidi uwezo, tena sana, lakini bado matumaini ya
kupata matokeo mazuri ugenini yalikuwapo, iwapo wachezaji wasingechoshwa
baada ya mchezo wa kwanza.
Ukifuatilia
ratiba ya Stars baada ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam ukalinganisha
na ya Algeria baada ya mchezo huo – kuelekea mchezo wa marudiano, huwezi
kustaajabu sana timu yetu ilicheza kichovu na kufungwa magoli mengi.
Kabla
ya kuanza kufikiria sababu nyingine zote, kuhujumiwa au fitina za
wenyeji, ukirudi kwenye ratiba ya timu baada ya mchezo wa kwanza
kuelekea mcheo mwingine, unagundua mchawi wa kwanza ni wahusika wa
timu.
Viongozi
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wale wa Kamati ya Taifa Stars
kwa kuipitisha timu safari ndefu kwenda Algiers kupitia Uturuki na vikao
vingi vilivyowanyima wachezaji japo muda wa kuutathmini mchezo wa
kwanza.
Ni
wazi wachezaji wa Taifa Stars walifika Algiers wakiwa wamechoka mwili
na akili na hawakuwa tayari kuhimili mchezo mwingine mgumu kuliko ule wa
Dar es Salaam.
Haya
ni mambo ambayo wakati tunajadili marefa na fitina za wenyeji, lazima
yajadiliwe pia ikiwa tunataka kufanya vizuri katika mashindano mengine.
Algeria wanaongeza silaha za vita, sisi tunazichosha silaha zetu kuelekea vitani.
Kama
Waalgeria walitufanyia figisu kuelekea mchezo wa marudiano, basi
hazikuwa na madhara makubwa kuliko fitina tulizojifanyia wenyewe.
Mpango
wa awali ulikuwa Taifa Stars isafiri na ndege ya kukodi ya Fats Jet
kwenda Algiers, ikawaje tena timu ikatumia ndege ya Uturuki?
Ndege ya kukodi siyo tu ingepunguza muda wa safari angani – bali pia ingetufanya tujipangie wenyewe ratiba yetu ya kuondoka.
Kuwanyima
wachezaji muda wa kupumzika na kuutathmini mchezo wa awali, ilikuwa ni
fitina nyingine mbaya ambayo tulijifanyia wenyewe pale Dar es Salaam.
Kwa
sasa tuseme yote.
Wanatuzidi uwezo. wametufanyia fitina. Lakini fitina
mbaya tulijifanyia wenyewe baada ya mchezo wa kwanza, kuelekea mchezo wa
marudiano Algiers. Inauma sana, lakini ndiyo hali halisi na hapa
unaweza kuwabaini watu wa kuwahusisha na matokeo haya mabaya.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatano, 18 Novemba 2015
MAONI YA MMOJA WA WANAKAMATI ILIYOUNDWA KUISAIDA TAIFA STARS
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni