Usiku wa November 17 watanzania wengi na
wapenzi wa soka walikuwa wakisubiri kuona mchezo wa pili wa marudiano
wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi kati ya timu ya taifa ya Algeria dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, mchezo ambao ulichezwa Blida Algeria katika uwanja wa Mustapha Tchaker.
Wakati Taifa Stars wanatafakari namna ambavyo watasawazisha magoli Mudathir Yahaya alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 41, kipindi cha pili kocha wa Tanzania Boniface Mkwasa alifanya mabadiliko ya kumuingiza Aishi Manula na kumtoa golikipa Aly Mustapha na Farid Mussa nafasi yake ikachuliwa na Salum Telela, mabadiliko ambayo hayakuzaa matunda.
Magoli ya Algeria yalifungwa na Yacine Brahimi dakika ya 1, Faouzi Ghoulam dakika ya 23 na dakika ya 59 akapachika goli jingine kwa mkwaju wa penati, Riyad Mahrez dakika ya 43 na Islam Slimani kafunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 49 na 75, Carl Medjani dakika ya 72 .
Kwa matokeo hayo Taifa Stars imetolewa kwa jumla ya magoli 9-2 baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
WAKATI HUOHUO;
KENYA
nayo imeungana na majirani Tanzania kuaga mbio za Kombe la Dunia 2018
nchini Urusi, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Cape Verde.
Matokeo hayo, yanaifanya Kenya itolewe kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya awali kushinda 1-0 nyumbani.
Mechi
nyingine, Rwanda imefungwa mabao 3-1 nyumbani na Libya, hivyo
kutolewa kwa jumla ya 4-1, baada ya awali kufungwa 1-0 ugenini.
Kongo imeifunga 2-1 Ethiopia, hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-4, baada ya awali kushinda 4-3, wakati Mali imeshinda 2-0 dhidi ya Botswana, hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 2-1.
Kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda (kushoto) ameshindwa kuisaidia timu yake mbele ya Libya |
Senegal imeifunga 3-0 Madagascar, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2 baada ya sare ya 2-2 awali, Burkina Faso imeshinda 2-0 dhidi ya Benin hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kufungwa 2-1.
Ivory Coast imeifunga 3-1 Liberia, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali kushinda 1-0.
Afrika
Kusini imeifunga 1-0 Angola hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa
4-1, baada ya awali kushinda 3-1, Tunisia imeifunga 2-1 Mauritania
hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya awali pia
kushinda 2-1.
Misri
imeifunga 4-0 Chad, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1
baada ya awali kufungwa 1-0, Ghana imeshinda 2-0 dhidi ya Comoro, hivyo
kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-0 baada ya sare ya 0-0 awali,
wakati Nigeria imeshinda 2-0 dhidi ya Swaziland na kusonga mbele 2-0
baada ya sare ya 0-0 awali na Cameroon imelazimishwa sare ya 0-0 na
Niger, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya ushindi
wa 3-0 awali.
Timu
hizo sasa zitagawanywa katika makundi matano na kumenyana katika mtindo
wa ligi, ambapo kinara wa kila kundi atafuzu Kombe la Dunia 2018.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni