Usiku wa jana ulikuwa ni wa aibu kwa Real Madrid na mashabiki wao,
huku mastaa wao Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wakishindwa kufanya
lolote la maana kuizuia Barcelona kupata ushindi mkubwa zaidi katika
dimba la Bernabeu tangu walipoifunga Madrid 6-2 chini ya utawala wa
Ronaldinho, Eto’o na Henry.
Wachezaji hao ghali zaidi duniani jana walikuwa na siku mbaya zaidi
katika historia yao ya kucheza EL Clasico – lakini mmoja wao alikuwa
flop zaidi ya mwenzie.
Mtandao wa takwimu za masuala ya michezo wa Opta
umetoa takwimu zao za mechi ya jana dhidi ya vijana wa Luis Enrique na
zipo kama ifuatavyo:
TAKWIMU ZA GARETH BALE VS BARCELONA
Katika mechi ya jana winga huyu wa Welsh aligusa mpira mara 41 tu,
akitengeneza nafasi 3, akapiga krosi 5 na kati hizo ni krosi moja tu
ndio iliyomfikia mlengwa – alipambana kushinda mpira kwa asilimia 25 tu
dhidi ya wachezaji wa timu pinzani.
TAKWIMU ZA CRISTIANO RONALDO VS BARCELONA
Mwanasoka bora wa dunia (mpaka January 2016) usiku wa El Clasico aligusa
mpira mara 46, akafanikiwa kutengeneza nafasi 1, akapiga krosi 1 ambayo
haikufanikiwa – lakini akashinda vita dhidi ya wapinzani kwa asilimia
53.
TAKWIMU ZA JUMLA
Wawili hawa ambao wote kwa pamoja waliigharimu Madrid kiasi cha £166m –
walicheza dakika 90 kila mmoja – Bale alipiga pasi 23, Ronaldo 29 –
usahihi wa pasi ulikuwa asilimia 73 kwa Bale na asilimia 89 kwa Ronaldo –
Bale alipiga mashuti 2 na Ronaldo 2, mashuti yaliyolenga goli – Bale 1,
Ronaldo yote mawili yalilenga goli kipa akaokoa.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumapili, 22 Novemba 2015
NANI ALIVURUNDA ZAIDI KATIKA EL CLASICO DHIDI YA BARCELONA?
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni