KIUNGO wa Manchester
City, Samir Nasri ametangaza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
wa Instagram kuwa hategemei kucheza mechi yeyote ya kimashindano katika
miezi mitatu ijayo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata majeruhi
ya msuli katika mchezo wa Ligi Kuu walioshinda mabao 5-1 dhidi ya
Bournemouth mwezi uliopita.
Meneja wa City, Manuel Pellegrini alikuwa na
matumaini kuwa Mfaransa huyo angeweza kurejea uwanjani katika mchezo
wao dhidi ya Liverpool mwishoni mwa wiki hii.
Lakini sasa matumaini hayo
yanaonekana kufifia baada ya kiungo huyo kuweka wazi hataweza kurejea
uwanjani mpaka Februari mwakani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni