Klabu ya Simba imetangaza kuwatema washambuliaji wake wawili, Pape N’daw na Simon Sserunkuma.
Ndani ya mechi nane, N’daw hajafunga hata bao moja, ameshindwa kuonyesha uwezo wake na ataendelea kukumbukwa na lile tukio la kukutwa na hirizi wakati Simba ikicheza na Prisons. Ni wazi klabu haijaona mchango wake wala kupata kile walichotarajia kutoka kwake, sasa basi.
Sserunkuma alisajiliwa msimu uliopita akitokea Uganda, lakini naye ameonyesha hakuna lolote. Ameshindwa kufanya kazi aliyoitiwa Msimbazi, hana ushawishi.
Wachezaji hao wa kigeni, walionekana hawana afaida yoyote katika kikosi cha Simba licha ya kupata utetezi wa mara kwa mara kutoka kwa benchi la ufundi likiamini huenda wangeweza kung'ara lakini ikawa kinyume.
Akizungumzia kuachwa kwa wachezaji hao Afisa habari wa msimbazi Simba HAJI MANARA amesema uongozi umeridhia na kuamua kuachana na wachezaji hao baada ya kupokea ripoti ya kocha Mkuu wa klabu hiyo DYRAN KERR kutowahitaji ndani ya kikosi chake kwa hivi sasa.
MANARA amesema pamoja na kuachana na wachezaji hao
klabu yao inamipango ya kuongeza wachezaji wengine ndani ya klabu hiyo katika
kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili hasa kumuongeza aliyekuwa mchezaji wao
PAUL KIONGERA na wachezaji wengine.
Kwa upande mwingine MANARA amefunguka kuhusu mipango
na maendeleo ya uwanja wao uliopo maeneo ya Bunju huku akiwapuuzi wale wanaoibeza
klabu hiyo kuhusu maendeleo ya uwanja wa klabu hiyo kushindwa kuujenga kwaajili
ya matumizi ya wachezaji wake.
Aidha klabu ya soka ya simba inaendelea na mazoezi
yake kwaajili ya mzunguko mwingine wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Wakati huo huo
Kiungo mshambuliaji Mcameroon
Doumbia Ernest ametua nchini akipambana kupata nafasi ya kuziba pengo la Pape N’daw
ambaye ametemwa rasmi.
Doumbia tayari
yuko jijini Dar es Salaam na anatarajia kuanza mazoezi leo akijifua na Simba
jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya majaribio na kama atafuzu, atasajiliwa wakati wa dirisha dogo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni