Kwa kila mfuatiliaji ama hata yule ambaye sio mfuatiliaji sana wa mieleka maarufu kama WWE (World Wrestling Entertainment) atakua anamfahamu Super Star John Cena.
John Cena ni kati ya wanamieleka bora zaidi wa muda wote katika historia ya WWE.
Lakini pamoja na mambo mengi makubwa ya ulingoni aliyokwisha yafanya gwiji huyu, pia ana mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa Total Divas anaitwa Nicole maarufu Nicky Bella.
Wawili hao walianza mahusiano yao miaka mitatu iliyopita na kiukweli Cena kakamatika. Sasa pamoja na mambo mengine ya kimahusiano, mchumba wake Nicole amekua akitamani kwa udi na uvumba kupata mtoto kutoka kwa staa huyo wa muda wote katika historia ya mieleka.
Lakini unajua John Cena kajibu nini kwa mpenziwe huyo baada ya kutamani wazae mtoto?? John anadai pamoja na kumpenda sana staa huyo mwenzake wa mieleka lakini hataki kuzaa naye wala kumuoa, anataka mapenzi tu.
Majibu hayo yanamuumiza kichwa Nicole Bella ambaye anatamani kuzaa mtoto lakini mpenziwe hana mpango. Lakini yuko staa mwingine anaitwa Dolph Zigler yeye anamzimia huyu binti na yuko tayari kumfanya mama, lakini Nicole naye anamzimia sana John, tusubiri kuona itakuaje baadae.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni