Usiku wa April 24 imetangazwa habari njema kwa soka la Afrika, baada ya winga mshambuliaji wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu ya Leicester City ya Uingereza Riyad Mahrez kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya PFA 2015/2016 (Professional Footballers Association) na kuwa Mwafrika pekee kufanikiwa kuchukua tuzo hiyo..
Riyad Mahrez ametangazwa kushinda tuzo hiyo mbele ya wachezaji kama Mesut Ozil wa Arsenal, Jamie Vardy wa Leicester City, Harry Kane wa Spurs, N’golo Kante wa Leicester City, Dimitri Payet wa West Ham United, PFA ni tuzo za wachezaji bora wa kulipwa.
Mahrez akizungumza baada ya kupoke tuzo pembeni kushoto ni kocha wake Claudio Ranieri
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Riyad Mahrez ndio alikuwa mchezaji wa Algeria aliyefunga goli la nne dakika ya 43 katika ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Taifa Stars November 17 2015 na kuIondoa Tanzania katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018.
Mahrez akifunga goli lake la 17 kwenye mchezo dhidi ya Swansea walipo pata ushindi wa 4-0
Jamie Vardy akikabidhiwa tuzo baada ya kuvifunga vilabu 11 mfululizo.
Vardy akiwa na tuzo yake baada ya kuvifunga vilabu 11 mfululizo katika ligi kiwa ni rekodi.
Kiungo chipukizi mwenye miaka 20 wa Tottenham, Dele Alli ambae mpaka hivi sasa ameshafunga magoli 10 na kutoa assist 9 mpaka hivi sasa amefanikiwa kushinda tuzo ya chipukizi bora wa msimu.
Mwingereza huyo amewashinda Ross Barkley,Romelu Lukaku wa Everton, goli kipa wa Stoke City Jack Butland,kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho na mchezaji mwenzake wa
Tottenham Kane.
Ryan Giggs amepewa tuzo ya heshima PFA Merit Award usoiku wa jana
Makocha hao ni Uingereza ( Roy Hodson),Wales (Chris Coleman), Northern Ireland (Michael O'Neill) na Martin O'Neill wa Republic of Ireland.
Mchezaji wa timu ya wanawake ya Manchester City Izzy Christiansen ameshinda tuzo ya PFA Women's player of the Year award
Mchezaji wa timu ya wanawake ya Sunderland Beth Mead ameshinda tuzo ya PFA Young Women's player of the Year award.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni