STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 23 Aprili 2016

BEKI JUMA ABDUL KAFANYA MAAMUZI JUU YA HATMA YAKE KLABUNI YANGA..........

 http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/07/yanga_logo_med_hr.jpeg

BEKI hodari wa kulia wa kimataifa wa Tanzania, Juma Abdul Jaffar Mnyamani amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC ya Dar es Salaam hadi mwaka 2018.
 
Habari kutoka ndani ya Yanga  zinasema kwamba Abdul alisaini Mkataba huo kabla ya timu hiyo kwenda Misri kucheza na Ahly.
 
Na hakuna kingine kilichoisukuma Yanga kumsainisha Mkataba mpya beki wake huyo zaidi ya kiwango chake kizuri kwa sasa akionekana kabisa kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini.

Juma Abdul (kushoto) amesaini Mkataba utakaomuweka Jangwani hadi 2018 

Na kwa kusaini Mkataba huo, Juma ataingia kwenye orodha ya wachezaji walioitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.
 
Juma aliyezaliwa Novemba 10, mwaka 1992
Mwananyamala, Dar es Salaam, alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea Mtibwa Sugar kwa Mkataba wa miaka miwili, ambao ulipoisha akaongezwa mwingine wa miaka miwili.
 
Na wakati Mkataba wake wa sasa unaelekea kumalizika mwishoni mwa msimu, inaelezwa tayari Juma Abdul amesaini Mkataba mwingine mpya wa miaka miwili utakaomfanya afikishe miaka sita Jangwani.
  
 
 SOURCE- BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox