STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 26 Aprili 2016

KWA MARA NYINGINE TENA SIMBA KUMEKUCHA YAMSIMAMISHA MCHEZAJI HUYU...........

SIMBA SC imemfungia kwa mwezi mmoja beki wake, anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Abdi Banda 

Simba imemfungia Banda tangu Aprili 1 na maana yake atakuwa huru kurejea kikosini mwishoni mwa mwezi huu.

 

Ofisa Habari wa Simba, Hajji Sunday Manara alisema suala la Banda litatolewa ufafanuzi  ili mchezaji huyo aweze kujua hatima Jumatano. “Kesho (Jumatano) tunakwenda kutoa uamuzi wa suala la Banda, tumekaa na kujadili utetezi wake, sasa tunatoa hukumu,”alisema Manara.

Banda alimgomea kocha Mganda, Jackson Mayanja kuingia dakika ya tano katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, kuchukua nafasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, akidai ni mapema mno kumtoa beki mwenzake kwa sababu ya makosa machache aliyofanya.
Baada ya mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 2-0, uongozi wa Simba alimtaka Banda kumuomba msamaha kocha Mayanja, lakini akagoma na tangu hapo hakuripoti mazoezini.

Baadaye Banda akatakiwa kuandika barua ya kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua kwa utovu wa nidhamu aliofanya, naye akafanya hivyo, ingawa Simba SC wamechukua muda mrefu kutoa uamuzi.






Barua ya Simba SC kumfungia kwa mwezi mmoja Abdi Banda
Chanzo: Bin Zubeir

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox