STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 22 Aprili 2016

RATIBA YA MICHUANO YA VIJANA INDIA YATOKA,SERENGETI BOYS KUFUNGUA NA MAREKANI.......


SHIRIKISHO la Soka India (AIFF) limetoa ratiba ya michuano ya vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) itakayoanza kutimua vumbi Mei 15 -25 katika mji wa Goa nchini India kwa Serengeti Boys kufungua dimba na Marekani.


   
Michuano ya AIFF inashirikisha timu tano za vijana wenye umri chini ya miaka 17 kutoka nchi za Korea Kusini, Marekani, Malysia, Tanzania na wenyeji India.

   

Mashindano hayo yatafanyika katika uwanja wa Tilak Maidan, Vasco, Goa kuanzia Mei 15, ambapo Tanzania itacheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Marekani, huku mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji India dhidi ya Malysia.
  Serengeti Boys watashuka dimbani tena Mei 17, kucheza na wenyeji India mchezo wa kwanza, Mei 19 Serengeti Boys watacheza dhidi ya Korea Kusini na mchezo wa mwisho watamaliza dhidi ya Malysia Mei 21.
  Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25 ambapo kabla ya mchezo wa fainali, utchezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa.
  Kikosi cha Serengeti Boys kianatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa mwezi Aprili, 2016 kujiandaa na michuano hiyo ya vijana na kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 mwakani nchini Madagascar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox