MUSTAKABALI
wa Mohamed Salah katika klabu ya Chelsea upo shakani, baada ya kutakiwa
kurejea nyumbani kwao, Msiri kuchukua mafunzo ya jeshi.
Salah,
aliyehamia Stamford Bridge kutoka Basle ya Uswisi Januari mwaka huu,
ameruhusiwa kuishi England kwa kigezo cha kushiriki masomo.
Pamoja
na hayo, usajili wake umesitishwa na Wizara ya Elimu ya Juu Misri,
tovuti ya soika ya www.kingfut.com imesema, maana yake mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 22 anaweza kurudi nchini mwao.
Ikiwa
Salah, aliyeichezea Chelsea mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Wimbledon
jana atatakiwa kurejea nyumbani, hataruhusiwa kuondoka tena Misri hadi
akamilishe mafunzo ya kijeshi, yanayochukua mwaka mmoja hadi mitatu.
"Salah ameelesea namna alivyoshitushwa juu ya uamuzi huu," amesema Mkurugenzi wa timu ya taifa ya Misri, Ahmed Hassan.
"Ameniambia anajaribu kuiwakilisha Misri katika njia nzuri zinazowezekana. Na haya ndiyo matokeo yake kutoka kwa nchi yake?'
Kikao
kinatarajiwa kufanyika baina ya FA ya Misri, benchi la ufundi la timu
ya taifa na Waziri wa Elimu ya Juu, kutafuta suluhisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni