Kivutio kipya: Luis Suarez akiwa amezingirwa na mashabiki mitaa ya Barcelona na mkewe Sofia Balbi
MSHAMBULIAJI Luis Suarez alizingirwa na mashabiki wakati akipita mitaa ya Barcelona na mkewe Sofia Balbi jana.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Uruguay aliyejiunga na klabu hiyo ya Katalunya
kutoka Liverpool kwa Pauni Milioni 75, alikuwa mwenye tabasamu pamoja na
familia yake wakati mashabiki wakimpokea kwa furaha.
Nyota
huyo wa zamani wa Wekundu wa Anfield aliyepigwa picha akisaini jezi ya
shabiki mmoja ya Lionel Messi - Suarez anatarajiwa kuwa pacha wa
Muargentina huyo msimu hiyo Nou Camp.
Suarez akisaini jezi ya shabiki mmoja wa Barcelona ya Lionel Messi jana mchana
Wakati
mashabiki kadhaa wa Barcelona walimzingira mchezaji wao huyo mpya,
Suarez hawezi kupata fursa ya kutambulishwa rasmi baada ya
kusajiliwa katokana na kufungiwa na FIFA kujihusisha na soka kwa meizi
minne kufuatia kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa
mechi baina ya Uruguay katika Kombe la Dunia nchini Brazil.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni