SHERMAN (KULIA) AKIWA NA MENEJA WA YANGA, HAFIDHI SALEH. |
Kpah Sherman amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga.
Mshambuliaji huyo raia wa Liberia amesaini mkataba wa kuichezea Yanga kwa miaka miwili leo jioni.
Mkataba wake mpya unaweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Liberia kuichezea Yanga.
Timu
pekee iliyowahi kuwa na mchezaji Mliberia ni Simba ambayo ilimiliki
William Fanbullar ambaye alikipiga kuanzia mwaka 1997 hadi 1999.
Tayari Sherman amefanya mazoezi mara mbili na kikosi chake cha Yanga na sasa yuko tayari kwa ajili ya mechi ya kesho.
Credit: Saleh Jembe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni