STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 4 Juni 2015

TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI 20 FIFA



"Tanzania (Taifa Stars) ilifanya vibaya katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) ilipofungwa kwa aibu katika hatua ya makundi dhidi ya timu vibonde vya Kundi B; Swaziland (1-0), Madagascar (2-0) na Lesotho (1-0)."
TANZANIA imeporomoka kwa nafasi 20 katika viwango vya ubora wa soka vya kila mwezi vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) leo.
Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa FIFA, Tanzania imeporomoka kutoka nafasi ya 107 iliyokuwa mwezi uliopita hadi nafasi ya 127 ambayo wamefungana na Vietnam.
Uganda wanaendelea kuongoza Afrika Mashariki wakiwa wameganda nafasi ya 71 duniani wakifuatwa na Rwanda (94), Kenya (123), Tanzania na Burundi (134).
10 bora barani Afrika imeendelea kuongozwa na Algeria ambao wameshuka kwa nafasi moja duniani hadi nafasi ya 21 wakifuatwa na Ivory Coast (24), Tunisia (29), Ghana (34), Senegal (36), Cape Verde (38), Nigeria (43), Guinea (45), Congo (47) na Cameroon 49).
Ujerumani imeendelea kuiongoza dunia ikifuatwa na Ubelgiji waliopanda kwa nafasi moja, Argentina, Colombia, Brazil, Uholanzi, Ureno, Uruguay, Ufaransa na Hispania wanaokamilisha 10 bora ya dunia.
Nchini hizo vibonde vilivyoing'oa Tanzania COSAFA 2015 zimepanda katika viwango hivyo vya ubora huku moja ikiporomoka.
Swaziland imepanda kwa nafasi 14 hadi nafasi ya 162, Madagascar imepanda kwa nafasi 37 hadi nafasi ya 113 wakati Lesotho imeshuka kwa nafasi moja ikiwa nafasi ya 122.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox