STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 18 Aprili 2016

EDEN HAZARD KAFUNGUKA JUU YA HATMA YAKE KLABUNI CHELSEA............



 


Eden Hazard amemwambia kocha anayekuja Chelsea Antonio Conte kwamba atasalia kwenye kikosi hicho licha ya kuwepo kwa taarifa zilizosambaa kwenye vyombo vya habari kwamba ataihama klabu hiyo.

 http://img0.cfstatic.com/wallpapers/c52773060b644a3aaa4d6b86aef1210a_large.png



Mbeligiji huyo ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Premier League amekuwa hayuko kwenye kiwango kizuri msimu huu huku akiwa bado hajafungia Chelsea goli hata moja kwenye meechi za EPL.


 




Hazard amekuwa akihusishwa kuhama Stamford Bridge  huku vilabu vya Real Madrid na Paris St-Germain kwa pamoja vikihusishwa kuitaka saini ya nyota huyo.

https://d.ibtimes.co.uk/en/full/1479731/guus-hiddink-discusses-eden-hazard-form.jpg




Lakini kwa mujibu wa gazeti la The Times, mshabuliaji huyo mwenye miaka 25 ambaye anamkataba wa miaka minne na The Blues, amemwambia boss wake ajaye kwamba anahitaji kuendelea kubaki Stamford Bridge kuliko kuondoka.
 


Kocha huyo wa kitaliano amefurahishwa na taarifa za Hazard kutaka kubaki na yuko tayari kumpa nafasi ya kuonesha makali yake kwenye kikosi atakachokiongoza.

Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa taji la EPL wapo nafasi ya 10 huku wakiwa wamesaliwa na michezo mitano, pointi 16 nyuma ya timu za top four.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox