STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 20 Aprili 2016

YANGA "OUT" YAFA KIUME MISRI, YACHAPWA 2-1 NA AL AHLY

YANGA SC imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly jana usiku  Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrFXsPVwO7KaipHy1FfwZyygUrlFPwfBY12s7Z7Q23yZoCWyr57e3OfKcJCFLD35Hc7rX0T2gmFgOsmQW-qdKw9E9sP4gQr7QGo6VZEU7scu76w4RUks06XhJeqI24OGXZhoFap-YoYjHf/s1600/DSC_1695.JPG Al Ahly inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
  Aliyewafungisha virago Yanga jana alikuwa ni Abdallah Said aliyefunga bao la pili dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kukamilika kwa dakika 90 za kawaida za mchezo akimalizia krosi ya  Walid Soliman kutoka upande wa kushoto.

Al Ahly walitangulia kupata bao katika mchezo huo kupitia kwa kiungo Hossam Ghaly aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Ahmed Fathi dakika ya 52.
 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma akaisawazishia Yanga dakika ya 57 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.

 
Kwa matokeo hayo, Yanga itamenyana na moja ya timu zilizofuzu Kombe la Shirikisho kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi.

 
Kwa Yanga, hii ni mara ya pili kufikia hatua hiyo baada ya mwaka 2007. Mwaka huo Yanga ilifungwa 3-0 na Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutoa sare 0-0 Mwanza.


ZILIZOFUZU NANE BORA LIGI YA MABINGWA;
Enyimba (Nigeria), Al Ahly (Misri), AS Vita (DRC), Asec Mimosas (Ivory Coast), Wydad Casablanca (Morocco), ES Setif (Algeria), Zamalek (Misri) na
Zesco United (Zambia).

 
ZILIZOANGUKIA KOMBE LA SHIRIKISHO;
ES Sahel (Tunisia), Yanga SC (Tanzania), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Ahly Tripoli (Libya), TP Mazembe (DRC), El Merreikh (Sudan), MO Bejaia (Algeria) na Stade Malien (Mali).

 
ZILIZOFUZU KOMBE LA SHIRIKISHO;
Kawkab Marrakech (Morocco), Mounana (Gabon), Misr Makkassa (Morocco), Medeama (Ghana), FAR Rabat (Morocco), Esperance (Tunisia), Sagrada Esperanca (Angola) na Stade Gabesien (Tunisia).

 
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk68, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Kevin Yondan dk86.

 
Al Ahly; Sherif Ekramy; Ahmed Fathi, Rami Rabia, Ahmed Hegazy, Sabri Rahil; Hossan Ashour, Hossam Ghaly, Hussein El Sayed, Moaem Zakaria/Walid Soliman dk64, Ramadan Sobhy na Amr Gamal/ Malick Evouna dk71.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox